إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّـٰجِدِينَ
Isipokuwa Ibilisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu
قَالَ يَـٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّـٰجِدِينَ
(Allah) alisema: Ewe Ibilisi! Umepatwa na nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?
قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُۥ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ
(Ibilisi) Alisema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliyemuumba kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope meusi yaliyovunda[1]
1- - Ibilisi aliyasema hayo kwa kiburi na kujiona kuwa, Yeye aliyeumbwa kwa miale ya moto ni bora
zaidi kuliko Yule aliyeumbwa kwa udongo mweusi, unaotoa sauti na uliovunda.
قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ
(Allah) alisema: Basi toka humo (Peponi), kwa hakika wewe ni umelaaniwa
وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na hakika laana itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
(Iblisi) Alisema: (Ewe) Mola wangu Mlezi, Nipe muhula (nibakishe) mpaka siku watakapofufuliwa (watu)
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
(Allah) alisema: Kwa hakika wewe ni katika waliopewa muhula (wa kutoangamizwa mpaka siku hiyo)
إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ
(Wewe utaendelea kuwepo) Mpaka siku ya wakati maalumu
قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
(Ibilisi) Alisema: (Ewe) Mola wangu Mlezi, kwa ulivyonipotoa, basi ninakuapia nitawapambia (upotovu) hapa duniani na nitawapoteza wote
إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipokuwa waja wako walio-safishwa
قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَيَّ مُسۡتَقِيمٌ
(Allah) Alisema: Hii Njia ya kuja kwangu Iliyo nyooka (kuwalinda waja wangu na upotovu hilo ni jukumu langu)
إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ
Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa (ataathirika nawe) yule mpotofu aliyekufuata
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Na bila shaka Jahanamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote (wanaokufuata)
لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٰبٖ لِّكُلِّ بَابٖ مِّنۡهُمۡ جُزۡءٞ مَّقۡسُومٌ
(Moto wa Jahanamu) una milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu waliyotengewa
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّـٰتٖ وَعُيُونٍ
Hakika wanaomuogopa Mola wao watakuwa katika Pepo na chemchem
ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ
(Wamchao Allah wataambiwa:) Ingieni (Peponi) kwa salama na amani
وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ
Na tutaondoa (kwa watu wa Peponi) chuki iliyokuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya fahari wakiwa wameelekeana
لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبٞ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ
Hautawagusa humo uchovu, wala humo hawatatolewa
۞نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Wape habari waja wangu ya kwamba, Mimi ndiye Mwenye kusamehe sana, Mwenye kurehemu
وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ ٱلۡعَذَابُ ٱلۡأَلِيمُ
Na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iliyo chungu mno
وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ
(Ewe Mtume) Na wape (waja wangu) habari za wageni wa Ibrahim
إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗا قَالَ إِنَّا مِنكُمۡ وَجِلُونَ
Walipoingia kwake na walisema: Salama! Yeye alisema (kwa kuingia kwenu bila kubisha hodi): Hakika sisi tunakuogopeni
قَالُواْ لَا تَوۡجَلۡ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ
Walisema (kumwambia): Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi mno (Naye ni Is-haka)
قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
(Ibrahimu) Alisema: Mnanibashiria (mwana) nami uzee umenishika![1] Basi mnanibashiria kwa kigezo gani?
1- - Ibrahimu hapa alileta mshangao unaotokana na muktadha wa ada na desturi za kibinadamu
kwamba, mtu kikongwe kama yeye ni nadra kupata mwana katika umri huo na si kupinga Qadari na
uweza wa Allah.
قَالُواْ بَشَّرۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡقَٰنِطِينَ
(Wale Malaika) Walisema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa (ya kupata mtoto uzeeni)
قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ
(Ibrahimu) Alisema: Na hakuna anayekata tamaa na rehema za Mola wake Mlezi isipokuwa wale (watu) waliopotea?
قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
(Ibrahimu) Alisema (zaidi ya bishara hii): Mna jambo gani lingine, enyi wajumbe?
قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ
Walisema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu (watu) waovu
إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Isipokuwa waliomfuata Lutwi (na kumuamini). Bila ya shaka sisi tutawaokoa wote
إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ
Ispokuwa mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni (mwa) watakaobakia nyuma