وَٱلطُّورِ
Nina apa kwa mlima wa Tur
وَكِتَٰبٖ مَّسۡطُورٖ
Na kwa kitabu kilichoandikwa
فِي رَقّٖ مَّنشُورٖ
Katika karatasi ya ngozi nyembamba iliyokunjuliwa
وَٱلۡبَيۡتِ ٱلۡمَعۡمُورِ
Na (nina apa) kwa Nyumba iliyoimarishwa (iliyojengwa imara)
وَٱلسَّقۡفِ ٱلۡمَرۡفُوعِ
Na (nina apa) kwa sakafu (za mbingu) zilizonyanyuliwa
وَٱلۡبَحۡرِ ٱلۡمَسۡجُورِ
Na (nina apa) kwa bahari yenye kuwashwa moto)
إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٞ
(Nina apa kwamba) Hakika, adhabu ya Mola wako Mlezi bila ya shaka yoyote itatokea
مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٖ
Hapana wa kuizuia
يَوۡمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوۡرٗا
Siku hiyo mbingu itatikisika kutikisika kikweli
وَتَسِيرُ ٱلۡجِبَالُ سَيۡرٗا
Na majabali yatatembea mwendo wa kasi
فَوَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Basi ole wao Siku hiyo kwa wakadhibishao
ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي خَوۡضٖ يَلۡعَبُونَ
Ambao wamo katika kushughulika na upuuzi wakicheza
يَوۡمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا
Siku watasukumwa katika Moto wa Jahannam kwa msukumo wa nguvu
هَٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
Huu ndio ule moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha
أَفَسِحۡرٌ هَٰذَآ أَمۡ أَنتُمۡ لَا تُبۡصِرُونَ
Je, hivi ni uchawi huu au nyinyi hamuoni?
ٱصۡلَوۡهَا فَٱصۡبِرُوٓاْ أَوۡ لَا تَصۡبِرُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡۖ إِنَّمَا تُجۡزَوۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Ingieni muungue humo kwenye Jahannam, mkistahamili au msistahamili ni sawasawa kwenu, hakika hapana ila mnalipwa yale mliyokuwa mkiyatenda
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّـٰتٖ وَنَعِيمٖ
Hakika ya wacha mungu watakua katika bustani na neema
فَٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ وَوَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ
Wakifurahia kwa ambayo Amewapa Mola wao, na Akawaokoa na adhabu ya moto uwakao vikali mno
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Kuleni na kunyweni kwa raha kwa sababu ya mliyokuwa mnatenda
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٖ مَّصۡفُوفَةٖۖ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٖ
Hali ya kuegemea juu ya makochi ya fakhari yaliyopangwa safu safu, na Tutawaozesha huwr ‘ayn, (wanawake weupe) wazuri wenye macho makubwa ya kupendeza
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱتَّبَعَتۡهُمۡ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَٰنٍ أَلۡحَقۡنَا بِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَمَآ أَلَتۡنَٰهُم مِّنۡ عَمَلِهِم مِّن شَيۡءٖۚ كُلُّ ٱمۡرِيِٕۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٞ
Na wale walioamini na wakafuatwa na dhuriya wao kwa Imani Tutawakutanisha nao dhuriya wao na Hatutawapunguzia katika ‘amali zao kitu chochote. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma
وَأَمۡدَدۡنَٰهُم بِفَٰكِهَةٖ وَلَحۡمٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ
Na Tutawapa matunda na nyama katika ambavyo wanatamani
يَتَنَٰزَعُونَ فِيهَا كَأۡسٗا لَّا لَغۡوٞ فِيهَا وَلَا تَأۡثِيمٞ
Watabadilishana humo gilasi za mvinyo usiosababisha maneno ya upuuzi na wala ya dhambi
۞وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ غِلۡمَانٞ لَّهُمۡ كَأَنَّهُمۡ لُؤۡلُؤٞ مَّكۡنُونٞ
Na watawazungukia watumishi vijana kwa ajili yao kana kwamba ni lulu zilizohifadhiwa
وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَسَآءَلُونَ
Na watakabiliana baadhi yao kwa wengine wakiulizana
قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا قَبۡلُ فِيٓ أَهۡلِنَا مُشۡفِقِينَ
Watasema hakika sisi tulikua kabla ya hapa kwa watu wetu wenye kuwafanyia upole
فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ
Basi Allah Akatufadhilisha, na Akatuokoa na adhabu ya mvuke wa moto (unaobabua)
إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلُ نَدۡعُوهُۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡبَرُّ ٱلرَّحِيمُ
Hakika sisi tulikuwa tunamuabudu kabla ya hapa hakika yeye ni mwema mwingi wa rehma
فَذَكِّرۡ فَمَآ أَنتَ بِنِعۡمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٖ وَلَا مَجۡنُونٍ
Basi kumbusha (Ewe Muhammad) na haukua wewe kwa neema ya mola wako mlezi kuhani wala mwendawazimu
أَمۡ يَقُولُونَ شَاعِرٞ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيۡبَ ٱلۡمَنُونِ
Au wanasema (huyu Muhammad þ ni) mshairi, tunamtarajia kupatikana maafa ya dahari