إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ
Hayo si chochote isipokuwa ni majina mmeyaita nyinyi na baba zenu, wala Allah Hakuyateremshia dalili yoyote. Hawafuati isipokuwa dhana na yale yanayotamani nafsi (zao), na hali imekwishawajia kutoka kwa Bwana wao mwongozo
وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُوَ يُدۡعَىٰٓ إِلَى ٱلۡإِسۡلَٰمِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anaye mzulia Allah uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Allah hawaongoi watu madhaalimu
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mkuu kabisa