السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 177

۞لَّيۡسَ ٱلۡبِرَّ أَن تُوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ قِبَلَ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡبِرَّ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ وَٱلۡكِتَٰبِ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ وَءَاتَى ٱلۡمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ ذَوِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِ وَٱلسَّآئِلِينَ وَفِي ٱلرِّقَابِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُوفُونَ بِعَهۡدِهِمۡ إِذَا عَٰهَدُواْۖ وَٱلصَّـٰبِرِينَ فِي ٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَحِينَ ٱلۡبَأۡسِۗ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْۖ وَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُتَّقُونَ

Sio wema peke yake kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni (wa) wanaomuamini Allah na Siku ya Mwisho na Malaika na Vitabu na Manabii, na wanatoa mali pamoja na kuwa wanaipenda wakawapa ndugu na mayatima na maskini na wasafiri na waombao na katika (kuwakomboa) watumwa, na wakawa wanasimamisha swala na kutoa zaka, na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na madhara na (katika) wakati wa vita. Hao ndio wa kweli na hao ndio wa mchao Allah



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 185

شَهۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٖ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهۡرَ فَلۡيَصُمۡهُۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٖ فَعِدَّةٞ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِكُمُ ٱلۡيُسۡرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ ٱلۡعُسۡرَ وَلِتُكۡمِلُواْ ٱلۡعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Ni mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imeteremshwa Qur’aniwe muongozo kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi. Basi atakayeshuhudia mwezi (huo) miongoni mwenu afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi[1] atimize hesabu katika siku nyingine[2]. Allah anakutakieni wepesi na hakutakieni uzito, na ili mumtukuze Allah kwa kukuongozeni na ili mpate kushukuru


1- - Anaruhusiwa kutofunga na kutimiza.


2- - Kwa kufunga zile siku ambazo hakufunga.