إِنَّ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika katika mbingu na ardhi ziko ishara kwa Waumini
وَفِي خَلۡقِكُمۡ وَمَا يَبُثُّ مِن دَآبَّةٍ ءَايَٰتٞ لِّقَوۡمٖ يُوقِنُونَ
Na katika umbo lenu na katika wanyama wanaotawanywa zimo ishara kwa watu wenye yakini
أَفَعَيِينَا بِٱلۡخَلۡقِ ٱلۡأَوَّلِۚ بَلۡ هُمۡ فِي لَبۡسٖ مِّنۡ خَلۡقٖ جَدِيدٖ
Je, kwani Tulichoka kwa uumbaji wa kwanza? Bali wao wamo katika shaka juu ya uumbaji upya (kufufuliwa)
أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
Au wameumbwa pasipo na kitu chochote (bila ya muumba) au wao ndio waumbaji?
ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ
Ambaye ameumba kifo na uhai ili akujaribuni; Ni nani miongoni mwenu mwenye kutenda (vitendo) vizuri zaidi? Na yeye (Allah) ndiye hasa Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kusamehe sana
ٱلَّذِي خَلَقَ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ طِبَاقٗاۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلۡقِ ٱلرَّحۡمَٰنِ مِن تَفَٰوُتٖۖ فَٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ هَلۡ تَرَىٰ مِن فُطُورٖ
Ambaye ameumba mbingu saba zilizo tabaka tabaka. Huoni tofauti yoyote katika uumbaji wa Rahmani (Allah Mwingi wa rehema). Basi rudisha macho (uangalie uumbaji wa Allah); Je, unaona kasoro yoyote?
ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا
Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا
Akainua kimo chake, na akaiten-geneza vizuri
وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا
Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake
وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
Na ardhi baada ya hayo Akai-tandaza
أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا
Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake
وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا
Na milima akaisimamisha,
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ
Hebu na ajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?