وَبَيۡنَهُمَا حِجَابٞۚ وَعَلَى ٱلۡأَعۡرَافِ رِجَالٞ يَعۡرِفُونَ كُلَّۢا بِسِيمَىٰهُمۡۚ وَنَادَوۡاْ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ أَن سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡۚ لَمۡ يَدۡخُلُوهَا وَهُمۡ يَطۡمَعُونَ
Na baina yao (baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni) kuna kizuizi (cha muinuko/ukuta). Na juu ya muinuko (huo) kuna watu wanaowafahamu wote (watu wa Peponi na wa Motoni) kwa alama zao. Na watu wa muinuko (huo) watawaita watu wa Peponi (na kuwaambia): “Amani iwe kwenu” huku hawajaingia humo na wana tamaa (ya kuingia)
۞وَإِذَا صُرِفَتۡ أَبۡصَٰرُهُمۡ تِلۡقَآءَ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِ قَالُواْ رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na (watu walioko kwenye muinuko) macho yao yatakapogeuzwa yatazame upande wa watu wa Motoni, watasema: “Ewe Mola wetu, usituweke pamoja na watu madhalimu”
وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَعۡرَافِ رِجَالٗا يَعۡرِفُونَهُم بِسِيمَىٰهُمۡ قَالُواْ مَآ أَغۡنَىٰ عَنكُمۡ جَمۡعُكُمۡ وَمَا كُنتُمۡ تَسۡتَكۡبِرُونَ
Na watu wa muinuko watawaita watu (wa Motoni) wanaowafahamu kwa alama zao na kuwaambia: “Haukukusaidieni wingi wenu wala hicho mlichokuwa mnafanyia kiburi