وَلَمَّا بَرَزُواْ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُواْ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Na walipotoka (hadharani) kupambana Na Jaluti Na majeshi yake, walisema: Mola wetu! Tumi-minie subira, na uiimarishe miguu yetu na utupe ushindi dhidi ya watu makafiri
فَهَزَمُوهُم بِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُۥدُ جَالُوتَ وَءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَهُۥ مِمَّا يَشَآءُۗ وَلَوۡلَا دَفۡعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لَّفَسَدَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Basi waliwashinda kwa idhini ya Allah na Daudi akamuua Jaluti, na Allah akampa (Daudi) ufalme na utume na akamfundisha aliyoyataka. Na kama Allah asingewakinga watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka ardhi ingeliharibika, lakini Allah ni Mwenye hisani kubwa mno kwa walimwengu
وَلَقَدۡ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ بِبَدۡرٖ وَأَنتُمۡ أَذِلَّةٞۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na hakika, Allah alikunusuruni katika vita vya Badri na ilhali nyinyi ni wanyonge. Basi mcheni Allah ili mshukuru (ili mpate daraja ya kuwa wenye kushukuru)
إِذۡ تَقُولُ لِلۡمُؤۡمِنِينَ أَلَن يَكۡفِيَكُمۡ أَن يُمِدَّكُمۡ رَبُّكُم بِثَلَٰثَةِ ءَالَٰفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ مُنزَلِينَ
Na (kumbuka) ulipowaambia Waumini: Hivi haitakutosheni Mola wenu kukuleteeni Malaika elfu tatu walioteremshwa?
بَلَىٰٓۚ إِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ وَيَأۡتُوكُم مِّن فَوۡرِهِمۡ هَٰذَا يُمۡدِدۡكُمۡ رَبُّكُم بِخَمۡسَةِ ءَالَٰفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ مُسَوِّمِينَ
Ni kweli kabisa; ikiwa mtakuwa na subira na mkamcha Allah na maadui wakakujieni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Mlezi atakuleteeni msaada wa Malaika elfu tano wenye kujiweka alama maalum
وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشۡرَىٰ لَكُمۡ وَلِتَطۡمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِۦۗ وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ
Na Allah hakufanya haya isipokuwa tu iwe bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate utulivu kwayo, na hakuna nusura isipokuwa kutoka kwa Allah tu, Mwenye nguvu kubwa, Mwingi wa hekima
لِيَقۡطَعَ طَرَفٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡ يَكۡبِتَهُمۡ فَيَنقَلِبُواْ خَآئِبِينَ
(Allah amefanya haya) Ili akate (aangamize) sehemu ya wale waliokufuru (kwa kuuawa vitani) au awafedheheshe wapate kurejea nyuma wakiwa hawakuambulia kitu
وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشۡرَىٰ وَلِتَطۡمَئِنَّ بِهِۦ قُلُوبُكُمۡۚ وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Na Allah hakulifanya (hili la kuleta vikosi vya Malaika) ila liwe bishara na ili kwalo nyoyo zenu zituwe (zitulizane). Na (ili hatimae mjue kwamba,) haupatikani ushindi ila kutoka kwa Allah tu. Hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima
لَقَدۡ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٖ وَيَوۡمَ حُنَيۡنٍ إِذۡ أَعۡجَبَتۡكُمۡ كَثۡرَتُكُمۡ فَلَمۡ تُغۡنِ عَنكُمۡ شَيۡـٔٗا وَضَاقَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ ثُمَّ وَلَّيۡتُم مُّدۡبِرِينَ
Kwa hakika kabisa, Allah (pamoja na uchache na udhaifu wenu) amekunusuruni katika maeneo mengi na (pia) siku ya Hunaini ambapo wingi wenu ulikufurahisheni (ulikuvimbisheni vichwa)[1] na (lakini wingi huo) haukukusaidieni kitu na ardhi, pamoja na wasaa wake, ikawa finyu kwenu. Kisha mkageuka nyuma (mkamuacha Mtume) mkikimbia
1- - Nyinyi mlikuwa elfu kumi na mbili na maadui wenu walikuwa elfu nne.
ثُمَّ أَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودٗا لَّمۡ تَرَوۡهَا وَعَذَّبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Kisha Allah akateremsha utulivu wake kwa Mtume wake na kwa Waumini, na akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona na akawaadhibu wale waliokufuru. Na hiyo ndio malipo ya makafiri
حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسۡتَيۡـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ كُذِبُواْ جَآءَهُمۡ نَصۡرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَآءُۖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُنَا عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
(Na hatukutuma kabla yako isipokuwa (Mitume) wanaume tunaowafunulia (tunaowashushia Wahyi) Mpaka Mitume (hao) walipokata tamaa (ya watu wao kutoamini) na wakadhani kuwa wamekadhibishwa (wamepingwa), hapo ikawajia nusura yetu natukawaokoa tuwatakao. Na adhabu yetu kali hairudishwi (haizuiliki) kwa watu waovu
أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَٰتَلُونَ بِأَنَّهُمۡ ظُلِمُواْۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ نَصۡرِهِمۡ لَقَدِيرٌ
Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Allah ni Muweza wa kuwasaidia
قَالَتۡ إِنَّ ٱلۡمُلُوكَ إِذَا دَخَلُواْ قَرۡيَةً أَفۡسَدُوهَا وَجَعَلُوٓاْ أَعِزَّةَ أَهۡلِهَآ أَذِلَّةٗۚ وَكَذَٰلِكَ يَفۡعَلُونَ
Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo
غُلِبَتِ ٱلرُّومُ
Warumi wameshindwa
فِيٓ أَدۡنَى ٱلۡأَرۡضِ وَهُم مِّنۢ بَعۡدِ غَلَبِهِمۡ سَيَغۡلِبُونَ
Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda
فِي بِضۡعِ سِنِينَۗ لِلَّهِ ٱلۡأَمۡرُ مِن قَبۡلُ وَمِنۢ بَعۡدُۚ وَيَوۡمَئِذٖ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
Katika miaka michache. Amri ni ya Allah tu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi
بِنَصۡرِ ٱللَّهِۚ يَنصُرُ مَن يَشَآءُۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Kwa nusura ya Allah, (Allah) anamnusuru amtakaye, na yeye tu ndiye Mwenye nguvu sana, Mwenye kurehemu sana
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡفَتۡحُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli?
قُلۡ يَوۡمَ ٱلۡفَتۡحِ لَا يَنفَعُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِيمَٰنُهُمۡ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ
Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula
إِنَّا فَتَحۡنَا لَكَ فَتۡحٗا مُّبِينٗا
Hakika tumekufungulia ushindi wa dhaahiri
وَيَنصُرَكَ ٱللَّهُ نَصۡرًا عَزِيزًا
Na (ili) Allah akunusuru nusura yenye nguvu kubwa
۞لَّقَدۡ رَضِيَ ٱللَّهُ عَنِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذۡ يُبَايِعُونَكَ تَحۡتَ ٱلشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَنزَلَ ٱلسَّكِينَةَ عَلَيۡهِمۡ وَأَثَٰبَهُمۡ فَتۡحٗا قَرِيبٗا
Kwa hakika Allah amewaridhia Waumini walipofungamana nawe (kwa kula Kiapo cha Utiifu) chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu.[1]
1- - Aya hii inawasifia Swahaba, Allah awawie radhi, kwa kupata radhi za Allah kwa kitendo chao cha kula Kiapo cha Utiifu (Baia) mbele ya Mtume wa Allah. Kama Allah amewapa radhi zake, jambo ambalo kila Muislamu analitamani, ni wazi kuwa watu hawa wanapaswa kuheshimiwa. Na hii ndio itikadi ya Ahlisuna Waljamaa (Suni).
وَمَغَانِمَ كَثِيرَةٗ يَأۡخُذُونَهَاۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمٗا
Na ngawira nyingi watakazo zichukua. Na Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima
وَعَدَكُمُ ٱللَّهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةٗ تَأۡخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمۡ هَٰذِهِۦ وَكَفَّ أَيۡدِيَ ٱلنَّاسِ عَنكُمۡ وَلِتَكُونَ ءَايَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ وَيَهۡدِيَكُمۡ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا
Allah anakuahidini ngawira nyingi mtakazo zichukua, basi amekutangulizieni hizi kwanza, na akaizuia mikono ya watu isikufikieni, na ili hayo yawe ni Ishara kwa Waumini, na akakuongozeni Njia Iliyo Nyooka
وَأُخۡرَىٰ لَمۡ تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهَا قَدۡ أَحَاطَ ٱللَّهُ بِهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٗا
Na mengine hamuwezi kuyapata bado, Allah amekwisha yazingia. Na Allah ni Muweza wa kila kitu
لَّقَدۡ صَدَقَ ٱللَّهُ رَسُولَهُ ٱلرُّءۡيَا بِٱلۡحَقِّۖ لَتَدۡخُلُنَّ ٱلۡمَسۡجِدَ ٱلۡحَرَامَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمۡ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَۖ فَعَلِمَ مَا لَمۡ تَعۡلَمُواْ فَجَعَلَ مِن دُونِ ذَٰلِكَ فَتۡحٗا قَرِيبًا
Hakika Allah amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah, kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na khofu. Yeye anajua msiyo yajua. Basi atakupeni kabla ya haya Ushindi karibuni
كَتَبَ ٱللَّهُ لَأَغۡلِبَنَّ أَنَا۠ وَرُسُلِيٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٞ
Allah Amekwishaandika kwamba: Bila shaka Nitashinda Mimi na Mitume Wangu. Hakika Allah ni Mwenye nguvu zote, Mwenye kushinda
وَأُخۡرَىٰ تُحِبُّونَهَاۖ نَصۡرٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتۡحٞ قَرِيبٞۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na kingine mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Allah, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!
إِذَا جَآءَ نَصۡرُ ٱللَّهِ وَٱلۡفَتۡحُ
Itakapokuja nusra ya Allah na ushindi (ukombozi wa mji wa Makka)