فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ
Wakaasi amri ya bwana wao, basi ikawachukua adhabu ya moto hali yakuwa wao wakiangalia
فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامٖ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ
Basi hawakuweza kusimama na hawakua wao wenye kushinda
وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ
Na Watu wa Thamuwd kisha Hakuwabakisha
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ
Kina Thamuwd waliwakadhibisha Waonyaji
فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٗا مِّنَّا وَٰحِدٗا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّفِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٍ
Wakasema: Ah! Tumfuate binaadamu miongoni mwetu? Hakika hapo sisi tutakuwa katika upotofu na wazimu
أَءُلۡقِيَ ٱلذِّكۡرُ عَلَيۡهِ مِنۢ بَيۡنِنَا بَلۡ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٞ
Ah! Ameteremshiwa ukumbusho (Wahyi) baina yetu? Bali yeye ni muongo mkubwa mwenye kiburi mno
سَيَعۡلَمُونَ غَدٗا مَّنِ ٱلۡكَذَّابُ ٱلۡأَشِرُ
Watakuja kujua kesho nani muongo mkubwa mwenye kiburi mno
إِنَّا مُرۡسِلُواْ ٱلنَّاقَةِ فِتۡنَةٗ لَّهُمۡ فَٱرۡتَقِبۡهُمۡ وَٱصۡطَبِرۡ
Hakika Sisi Tutawapelekea ngamia jike awe jaribio kwao, basi (Ee Nabiy Swaalih) watazame na vuta subira
وَنَبِّئۡهُمۡ أَنَّ ٱلۡمَآءَ قِسۡمَةُۢ بَيۡنَهُمۡۖ كُلُّ شِرۡبٖ مُّحۡتَضَرٞ
Na wajulishe kwamba maji ni mgawanyo baina yao (ngamia na wao), kila sehemu ya maji itahudhuriwa (kwa zamu)
فَنَادَوۡاْ صَاحِبَهُمۡ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ
Wakamuita Mtu Wao Akajipa Ushujaa Na Kumchinja
فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi Vipi Ilikua Adhabu Yangu Na Maonyo yangu?
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَكَانُواْ كَهَشِيمِ ٱلۡمُحۡتَظِرِ
Hakika Sisi Tulipeleka Kwao Ukelele Moja tu, wakawa kama mabuwa yaliyokatika-katika ya mtengenezaji zizi
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ
Kina Thamudi na Adi walikadhibisha tukio (Kiyama) lenye kugonga (na kutia kiwewe)
فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ
Ama kina Thamudi, waliangamizwa kwa ukelele mkali sana
وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ
Na ama kina Adi, waliangamizwa kwa upepo wenye baridi kali, uvumao kwa nguvu
سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ
(Allah) Aliwapelekea mausiku saba na michana minane mfululizo (bila kupumzika). Basi utaona watu wameanguka kifudifudi kana kwamba ni magogo ya mitende yaliyo wazi ndani
فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ
Basi je, unamuona yeyote aliyebaki?
وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ
Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ
Kina Thamudi walikadhibisha kwasababu ya upotofu wao,
إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا
Alipo simama mwovu wao mkubwa
فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا
Hapo Mtume wa Allah alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Allah, mwacheni anywe maji fungu lake
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwahivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwasababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa
وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا
Wala Yeye haogopi matokeo yake