مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
Mmiliki wa Siku ya Malipo
كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوۡنَ أُجُورَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۖ فَمَن زُحۡزِحَ عَنِ ٱلنَّارِ وَأُدۡخِلَ ٱلۡجَنَّةَ فَقَدۡ فَازَۗ وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا مَتَٰعُ ٱلۡغُرُورِ
Kila nafsi itaonja kifo, si vingine malipo yenu mtapewa yakiwa kamili siku ya kiyama, atakaye epushwa na kuwekwa mbali na Moto na akaingizwa Peponi basi huyo amefanikiwa, na haikua maisha ya dunia ila ni starehe zenye kudanganya
وَٱلَّذِيٓ أَطۡمَعُ أَن يَغۡفِرَ لِي خَطِيٓـَٔتِي يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo
وَقَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا هَٰذَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyokuwa mnaikadhibisha
يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Wanauliza Ni Lini Hiyo Siku Ya Malipo
يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ
Siku Hiyo Wao Katika Moto Watachomwa
ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ
Onjeni Adhabu Yenu Hii Ambayo Mlikua Kwayo Mnaiharakisha
وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Wataingia humo Siku ya Malipo
وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ
Na hawatoacha kuwamo humo
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ
(Ni) Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu