إِنَّا جَعَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ
Hakika, Sisi tumekifanya (hicho kitabu) Qur’ani ya Kiarabu ili mfahamu
وَإِنَّهُۥ فِيٓ أُمِّ ٱلۡكِتَٰبِ لَدَيۡنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ
Na hakika kitabu hicho katika Kitabu Mama kilichopo kwetu, kwa yakini kabisa, ni kitukufu, chenye hekima nyingi
وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ
Nina apa kwa Kitabu kinacho bainisha
إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
Hakika, tumekiteremsha (kitabu hiki cha Qur’ani) katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi tumekuwa waonyaji
تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ
(Huu) Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allah, Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana
تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَ ٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ يُؤۡمِنُونَ
Hizo Aya za Allah tunakusomea kwa haki. Basi ni mazungumzo gani watayaamini baada ya Allah na Aya zake?
تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ
(Huu) Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allah, Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana
إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ
Hakika ya hiyo ni Kurani tukufu
فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ
Katika Kitabu kilichohifadhiwa
لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ
Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa (Walio twahara)
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ni uteremsho kutoka kwa Mola wa walimwengu wote
هُوَ ٱلَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبۡدِهِۦٓ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖ لِّيُخۡرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ بِكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ
Yeye Ndiye Yule Anayemte-remshia mja Wake Aya zinazo bainisha ili Akutoeni katika giza na kukuingizeni kwenye Nuru. Na hakika Allah kwenu ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ni Uteremsho Kutoka Kwa Mola Wa Viumbe Vyote
إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ تَنزِيلٗا
Hakika Sisi tumekuteremshia Qur’ani kidogo kidogo (hatua kwa hatua)