إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ
Hakika Allah ndiye yeye mtoa riziki mwenye nguvu kubwa
وَيَرۡزُقۡهُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَحۡتَسِبُۚ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسۡبُهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَٰلِغُ أَمۡرِهِۦۚ قَدۡ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَيۡءٖ قَدۡرٗا
Na humruzuku kwa njia asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Allah Yeye humtosha. Hakika Allah anatimiza amri yake. Hakika Allah Amejaalia kwa kila kitu na makadirio yake
أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي يَرۡزُقُكُمۡ إِنۡ أَمۡسَكَ رِزۡقَهُۥۚ بَل لَّجُّواْ فِي عُتُوّٖ وَنُفُورٍ
Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanaendelea (wanang’ang’ania) tu katika jeuri na chuki
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo