وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ
Na maji yenye kumiminwa
وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ
Na matunda mengi
لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ
Hayana kikomo na wala hayakatazwi
وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ
Na matandiko ya kupumzikia yaliyoinuliwa
إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ
Hakika Sisi Tutawaumba (Mahurulaini) upya
فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا
Na tukawafanya kuwa bikra
عُرُبًا أَتۡرَابٗا
Wenye mahaba kwa waume zao, na wana umri unaolingana
لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Ni kwaajili ya watu wa kuliani
سَابِقُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا كَعَرۡضِ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أُعِدَّتۡ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۚ ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ
Kimbilieni kuomba msamaha kwa Mola wenu na Pepo (ambayo) upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale walio muamini Allah na Mtume Wake. Hiyo ni fadhila ya Allah, Humpa Amtakaye. Na Allah ni Mwenye fadhila kubwa
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ
Katika Bustani (Pepo) Iliyo Juu,
قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ
Vishada Vyake (vya matunda) Vitakuwa Karibu:
وَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُواْ جَنَّةٗ وَحَرِيرٗا
Na Atawalipa kwasababu ya kusubiri kwao, Pepo na nguo za hariri
مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۖ لَا يَرَوۡنَ فِيهَا شَمۡسٗا وَلَا زَمۡهَرِيرٗا
Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona (hawatahisi) humo jua kali wala baridi kali.[1]
1- - Aya ni dalili kuwa Akhera kuna adhabu ya Baridi. Kama alivyopokea Imamu Bukhariy na Muslim- kutoka kwa Abuu Hurairah –(Allah amuwiye radhh) amesema; amesema Mtume wa Allah (Rehema na amani ziwe juu yake):-
وَدَانِيَةً عَلَيۡهِمۡ ظِلَٰلُهَا وَذُلِّلَتۡ قُطُوفُهَا تَذۡلِيلٗا
Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning’inia mpaka chini
وَيُطَافُ عَلَيۡهِم بِـَٔانِيَةٖ مِّن فِضَّةٖ وَأَكۡوَابٖ كَانَتۡ قَوَارِيرَا۠
Na watazungushiwa vyombo vya fedha, na bilauri zilokuwa za vigae
قَوَارِيرَاْ مِن فِضَّةٖ قَدَّرُوهَا تَقۡدِيرٗا
Vigae safi kutokana na fedha wamezipima kwa kipimo
وَيُسۡقَوۡنَ فِيهَا كَأۡسٗا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا
Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi
عَيۡنٗا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلۡسَبِيلٗا
Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil
۞وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيۡتَهُمۡ حَسِبۡتَهُمۡ لُؤۡلُؤٗا مَّنثُورٗا
Na watawazungukia wavulana wasio pevuka wakiwatumikia, ukiwaona utadhani ni lulu zilizo tawanywa
وَإِذَا رَأَيۡتَ ثَمَّ رَأَيۡتَ نَعِيمٗا وَمُلۡكٗا كَبِيرًا
Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa
عَٰلِيَهُمۡ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضۡرٞ وَإِسۡتَبۡرَقٞۖ وَحُلُّوٓاْ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٖ وَسَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ شَرَابٗا طَهُورًا
Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya atilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao atawanywesha kinywaji safi kabisa
إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمۡ جَزَآءٗ وَكَانَ سَعۡيُكُم مَّشۡكُورًا
(Wataambiwa) Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa
إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا
Hakika wacha Mungu wanastahiki kufuzu
حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبٗا
[watapata] Mabustani na mizabibu
وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابٗا
Na wake wenye vifua vya kujaa, na walio lingana nao
وَكَأۡسٗا دِهَاقٗا
Na bilauri zilizo jaa,
لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا كِذَّـٰبٗا
Hawatasikia humo upuuzi wala uongo
جَزَآءٗ مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابٗا
Hali yakuwa ni Malipo kutoka kwa Mola wako, ni kipawa cha kutosha
يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ
Watanyweshwa kinywaji safi kilichotiwa muhuri,
خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana