ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauna, hakika yeye amepindukia mipaka
فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
Umwambie: Je, unataka utakasike?
وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ
Na nikuongoze kwa Mola wako umuogope?
فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi akamuonyesha Ishara (muujiza) mkubwa kabisa
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
Lakini aliikadhibisha na akaasi
ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ
Kisha akageuka nyuma na kufanya juhudi, (ya kukanusha)
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
Akakusanya watu akatangaza
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mkuu kabisa
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ
Basi hapo Allah akamshika na kumuadhibu kwa adhabu ya mwisho na mwanzo.[1]
1- - Allah akampa adhabu kwa kauli yake ya mwisho, nayo ni vile kusema: “Mimi ndiye Mola wenu Mlezi aliye mkubwa kabisa. Na akampa adhabu kwa kauli yake ya mwanzo, nayo ni kumkadhibisha Musa”.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ
Hakika katika hayo bila shaka kuna funzo kwa yule anayeogopa