إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٖ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكٗا وَهُدٗى لِّلۡعَٰلَمِينَ
Kwa yakini kabisa, nyumba ya kwanza kabisa kuwekwa (ardhini) kwa ajili ya watu (ili kumuabudu Allah) ni ile (Alkaaba) iliyoko Makkah ikiwa imebarikiwa na ni uongofu kwa walimwengu wote
وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِيمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا ٱلۡبَلَدَ ءَامِنٗا وَٱجۡنُبۡنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعۡبُدَ ٱلۡأَصۡنَامَ
Na (kumbuka) Ibrahim alipo-sema: Ewe Mola wangu Mlezi, ujaalie mji huu uwe wa amani (kwa watu, mimea na wanyama) na uniepushe mimi na wanangu kuabudu masanamu
رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضۡلَلۡنَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُۥ مِنِّيۖ وَمَنۡ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Ewe Mola wangu Mlezi, hakika hayo (masanamu) yamewapoteza watu wengi mno. Basi kwa aliyenifuata mimi huyo ni wangu, na aliyeniasi, hakika Wewe ni Mwenye kusamehe mwenye kurehemu
رَّبَّنَآ إِنِّيٓ أَسۡكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيۡرِ ذِي زَرۡعٍ عِندَ بَيۡتِكَ ٱلۡمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱجۡعَلۡ أَفۡـِٔدَةٗ مِّنَ ٱلنَّاسِ تَهۡوِيٓ إِلَيۡهِمۡ وَٱرۡزُقۡهُم مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡكُرُونَ
Mola wetu Mlezi, hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuriya zangu (Ismaili na mama yake) kwenye bonde lisilokuwa na mimea, kwenye Nyumba yako Takatifu, ewe Mola wetu Mlezi, ili wasimamishe Swala. Basi zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao, na waruzuku kila aina ya matunda, ili wapate kushukuru
لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Naapa kwa Mji huu!
وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Nawe unakaa Mji huu
وَهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٱلۡأَمِينِ
Na mji huu (wa Makka) wenye amani