يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡمَلِكِ ٱلۡقُدُّوسِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ
Vinamtakasa Allah (viumbe) vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi, Mfalme, Mtukufu, Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana
يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Vinamsabihi Allah (viumbe) vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Ni wake yeye tu ufalme na ni zake yeye tu sifa njema. Na Yeye ni Mwenye uwezawa kila kitu
تَبَٰرَكَ ٱلَّذِي بِيَدِهِ ٱلۡمُلۡكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Ametakasika (Allah) Ambaye ufalme umo mikononi Mwake yeye tu, Naye ni Muweza sana wa kila kitu
ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Allah ni shaahidi wa kila kitu
مَلِكِ ٱلنَّاسِ
Mfalme wa watu