مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ يَهۡدِ قَلۡبَهُۥۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ
Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah. Na mwenye kumuamini Allah huuongoa moyo wake. Na Allah ni Mjuzi wa kila kitu
ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّۖ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَهُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عِلۡمَۢا
Allah ndiye yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Allah ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba Allah amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa elimu yake
وَأَسِرُّواْ قَوۡلَكُمۡ أَوِ ٱجۡهَرُواْ بِهِۦٓۖ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Na fanyeni siri kauli zenu, au zidhihirisheni, hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani
قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡعِلۡمُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allah; na hakika mimi ni muonyaji tu mwenye kubainisha
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ
Hakika, Mola wako Mlezi ndiye amjuae zaidi aliyepotea njia yake, ndiye awajuae zaidi walioongoka
وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَـٰٓئِكَةٗۖ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَهُمۡ إِلَّا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَٰنٗا وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡكَٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ
Na Hatukuweka walinzi wa moto isipokuwa ni Malaika, na Hatukufanya idadi yao isipokuwa iwe ni mtihani kwa wale waliokufuru; ili wawe na yakini wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie Imani wale walioamini; na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini; na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki), na makafiri waseme: Allah Amekusudia nini kwa mfano huu? Hivyo ndivyo Allah Anavyompoteza Amtakaye na Anamuongoa Amtakaye. Na hakuna ajuaye majeshi ya Mola wako isipokuwa Yeye Peke yake, na haya hayakuwa isipokuwa ni ukumbusho tu kwa binadamu
وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ
Na Allah anajua wanayo yadhamiria
إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ
Ila akipenda Allah. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana