ٱذۡهَبُواْ بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلۡقُوهُ عَلَىٰ وَجۡهِ أَبِي يَأۡتِ بَصِيرٗا وَأۡتُونِي بِأَهۡلِكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Nendeni na kanzu yangu hii na mkaitupie usoni kwa Baba yangu, (akiipata harufu yangu tu atapona na) ataona na nileteeni familia yenu yote
وَلَمَّا فَصَلَتِ ٱلۡعِيرُ قَالَ أَبُوهُمۡ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَۖ لَوۡلَآ أَن تُفَنِّدُونِ
Na msafara ulipoondoka tu (Misri), Baba yao alisema (kuwaambia aliokuwa nao): Hakika, mimi kwa yakini kabisa nanusa harufu ya Yusuf, lau kama hamtaniona mpuuzi
قَالُواْ تَٱللَّهِ إِنَّكَ لَفِي ضَلَٰلِكَ ٱلۡقَدِيمِ
Walisema: Tunaapa kwa Allah, hakika wewe bado kabisa ungali katika upotevu wako wa kale (wa kumpenda Yusuf)
فَلَمَّآ أَن جَآءَ ٱلۡبَشِيرُ أَلۡقَىٰهُ عَلَىٰ وَجۡهِهِۦ فَٱرۡتَدَّ بَصِيرٗاۖ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Basi alipofika mbashiri na akaitupa kanzu usoni kwake na kwasababu hiyo, akarejea kuona, alisema: Je, sikukuambieni kuwa mimi ninajua kwa Allah msiyoyajua?
قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَا ٱسۡتَغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَآ إِنَّا كُنَّا خَٰطِـِٔينَ
Walisema: Ewe Baba yetu, tuombee (kwa Allah) msamaha kwa dhambi zetu. Kwa hakika sisi tulikuwa wakosaji
قَالَ سَوۡفَ أَسۡتَغۡفِرُ لَكُمۡ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
Alisema: Nitakuombeeni msa-maha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika, Yeye (Allah) ndiye tu Msamehevu, Mwenye kurehemu
فَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيۡهِ أَبَوَيۡهِ وَقَالَ ٱدۡخُلُواْ مِصۡرَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ
Basi walipoingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na alisema: Ingieni Misri, Inshaa-Allah, mkiwa katika amani
وَرَفَعَ أَبَوَيۡهِ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ وَخَرُّواْ لَهُۥ سُجَّدٗاۖ وَقَالَ يَـٰٓأَبَتِ هَٰذَا تَأۡوِيلُ رُءۡيَٰيَ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَعَلَهَا رَبِّي حَقّٗاۖ وَقَدۡ أَحۡسَنَ بِيٓ إِذۡ أَخۡرَجَنِي مِنَ ٱلسِّجۡنِ وَجَآءَ بِكُم مِّنَ ٱلۡبَدۡوِ مِنۢ بَعۡدِ أَن نَّزَغَ ٱلشَّيۡطَٰنُ بَيۡنِي وَبَيۡنَ إِخۡوَتِيٓۚ إِنَّ رَبِّي لَطِيفٞ لِّمَا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi, na wote wakaporomoka kumsujudia.[1] Na (Yusuf) alisema: Ewe Baba yangu, hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu pale zamani. Na Allah ameijaalia (ndoto hiyo) kuwa ya kweli. Na (Allah) amenifanyia mazuri mno kwasababu alinitoa gerezani na amekuleteni kutoka jangwani baada ya shetani kuchochea uhasama baina yangu na baina ya ndugu zangu. Hakika, Mola wangu Mlezi ni Muungwana kwa ayatakayo. Kwa hakika, Yeye (Allah) ndiye Mjuzi, Mwenye hekima
1- - Huu ulikuwa utaratibu wa wakati huo wa kusalimia viongozi kwa kusujudu.
۞رَبِّ قَدۡ ءَاتَيۡتَنِي مِنَ ٱلۡمُلۡكِ وَعَلَّمۡتَنِي مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِۚ فَاطِرَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ أَنتَ وَلِيِّۦ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ تَوَفَّنِي مُسۡلِمٗا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّـٰلِحِينَ
(Kisha Yusuf akaomba akasema): Ewe Mola wangu Mlezi, kwa hakika umenipa sehemu ya ufalme na umenifundisha sehemu ya tafsiri ya matukio (ndoto). (Ewe) Muumba wa mbingu na ardhi, Wewe ndiye Mlinzi wangu duniani na Akhera. Nifishe nikiwa Muislamu na nikutanishe na wenye kutenda mema