السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 70

قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ ٱلۡبَقَرَ تَشَٰبَهَ عَلَيۡنَا وَإِنَّآ إِن شَآءَ ٱللَّهُ لَمُهۡتَدُونَ

Wakasema: Tuulizie (kwa) Mola wako atubainishie kuwa yuko vipi? Hakika ng’ombe wametuchanganya (kwa kufanana), nasi Allah akipenda tutaongoka



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 71

قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا ذَلُولٞ تُثِيرُ ٱلۡأَرۡضَ وَلَا تَسۡقِي ٱلۡحَرۡثَ مُسَلَّمَةٞ لَّا شِيَةَ فِيهَاۚ قَالُواْ ٱلۡـَٰٔنَ جِئۡتَ بِٱلۡحَقِّۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُواْ يَفۡعَلُونَ

Akasema: Allah anasema kuwa ni ng’ombe asiyetumikishwa kwa kazi ya kulima wala kumwagilia mashamba. Awe salama; asiwe na kasoro katika mwili wake. Wakasema: Sasa umekuja na haki. Basi wakamchinja na walikaribia kutotekeleza



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 72

وَإِذۡ قَتَلۡتُمۡ نَفۡسٗا فَٱدَّـٰرَٰٔتُمۡ فِيهَاۖ وَٱللَّهُ مُخۡرِجٞ مَّا كُنتُمۡ تَكۡتُمُونَ

Na (kumbukeni enyi Wana wa Israeli) mlipoua nafsi (mtu) kisha mkatafautiana katika hilo, na Allah ni mwenye kuyatoa hayo mliyokuwa mkiyaficha



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 73

فَقُلۡنَا ٱضۡرِبُوهُ بِبَعۡضِهَاۚ كَذَٰلِكَ يُحۡيِ ٱللَّهُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَيُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Tukasema: Mpigeni huyo ng’ombe kwa sehemu yake. Ni kama hivyo Allah anawafufua waliokufa, na anakuonesheni aya zake ili mpate kuweka mambo akilini



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 74

ثُمَّ قَسَتۡ قُلُوبُكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَٱلۡحِجَارَةِ أَوۡ أَشَدُّ قَسۡوَةٗۚ وَإِنَّ مِنَ ٱلۡحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنۡهُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخۡرُجُ مِنۡهُ ٱلۡمَآءُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَهۡبِطُ مِنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Kisha mioyo yenu ikawa migumu; ikawa kama jiwe au migumu zaidi (yajiwe). Kwa hakika, katika mawe yapo ambayo mito hububujika kutokea humo, na pia katika hayo mawe yapo ambayo hupasuka na maji yakatoka humo, na pia katika mawe yapo ambayo huporomoka kutokana na kumuogopa Allah. Na Allah si mwenye kughafilika na hayo mnayoyafanya



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 75

۞أَفَتَطۡمَعُونَ أَن يُؤۡمِنُواْ لَكُمۡ وَقَدۡ كَانَ فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ يَسۡمَعُونَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُۥ مِنۢ بَعۡدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

“Je, hivi mnatumai kuwa watakufuateni katika imani na ilhali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Allah, kisha wanayapotosha baada yakuwa wameyafahamu vizuri, na ilhali wanajua.[1]


1- - Kuwa wanachofanya ni upotoshaji?


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 76

وَإِذَا لَقُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ قَالُوٓاْ أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ لِيُحَآجُّوكُم بِهِۦ عِندَ رَبِّكُمۡۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na wakikutana na walioamini wanasema: Nasi pia tumeamini. Na wanapokuwa peke yao husema wakiambizana kuwa: Hivi mnawaambia yale aliyoyafunua Allah kwenu ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Mola wenu? Hivi nyinyi hamna akili?



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 77

أَوَلَا يَعۡلَمُونَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَ

Hivi hawajui kwamba Allah anayajua wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha?



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 78

وَمِنۡهُمۡ أُمِّيُّونَ لَا يَعۡلَمُونَ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّآ أَمَانِيَّ وَإِنۡ هُمۡ إِلَّا يَظُنُّونَ

Na miongoni mwao wapo wajinga wasiojua (kusoma) kitabu isipokuwa (wanachojua ni) matumaini tu, na hawakuwa wao ila ni watu wanao-fuata dhana tu



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 79

فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ يَكۡتُبُونَ ٱلۡكِتَٰبَ بِأَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ يَقُولُونَ هَٰذَا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ لِيَشۡتَرُواْ بِهِۦ ثَمَنٗا قَلِيلٗاۖ فَوَيۡلٞ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتۡ أَيۡدِيهِمۡ وَوَيۡلٞ لَّهُم مِّمَّا يَكۡسِبُونَ

Basi ole wao wanaoandika maandishi kwa mikono yao kisha wanasema kuwa (maandishi) hayo yanatoka kwa Allah, ili kwa kufanya hivyo wabadilishe kwa lengo la kupata pato dogo. Basi ole wao kwa kile kinachoandikwa kwa mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyafanya



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 80

وَقَالُواْ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامٗا مَّعۡدُودَةٗۚ قُلۡ أَتَّخَذۡتُمۡ عِندَ ٱللَّهِ عَهۡدٗا فَلَن يُخۡلِفَ ٱللَّهُ عَهۡدَهُۥٓۖ أَمۡ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Na walisema: Moto (wa Jaha-namu) hautatugusa (hautatuunguza) isipokuwa (kwa) siku chache tu zenye kuhesabika. Sema (uwaulize): Je, mna ahadi kwa Allah juu ya hilo na kwamba Allah hatavunja ahadi yake? Au mnamsingizia Allah mambo msiyoyajua?



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 81

بَلَىٰۚ مَن كَسَبَ سَيِّئَةٗ وَأَحَٰطَتۡ بِهِۦ خَطِيٓـَٔتُهُۥ فَأُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Hali si kama wanavyodai. (Hali iko hivi): Wote watendao dhambi na dhambi zao zikawazunguka[1] hao ndio watu wa Motoni; wataishi humo milele


1- - Wakabobea katika kutenda dhambi.


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 82

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na walioamini na wakatenda yaliyo mema hao ndio watu wa Peponi; wataishi humo milele



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 83

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ لَا تَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَانٗا وَذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَقُولُواْ لِلنَّاسِ حُسۡنٗا وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنكُمۡ وَأَنتُم مُّعۡرِضُونَ

Na (kumbukeni) Tulipochukua ahadi kwa Wana wa Israeli kwamba, hamtamuabudu yeyote Ila Allah tu, na mtawatendea wema wazazi, na ndugu na yatima na maskini, na mseme na watu kwa maneno mazuri. Na simamisheni Swala na toeni Zaka, kisha mkakengeuka isipokuwa wachache tu kati yenu, na ilhali nyinyi mnapuuza



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 84

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ لَا تَسۡفِكُونَ دِمَآءَكُمۡ وَلَا تُخۡرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ ثُمَّ أَقۡرَرۡتُمۡ وَأَنتُمۡ تَشۡهَدُونَ

Na (kumbukeni) tulipochukua ahadi kwenu kwamba msimwage damu zenu, wala msiwatoe watu wenu katika nyumba zenu, nanyi mkakubali ilhali mnashuhudia



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 85

ثُمَّ أَنتُمۡ هَـٰٓؤُلَآءِ تَقۡتُلُونَ أَنفُسَكُمۡ وَتُخۡرِجُونَ فَرِيقٗا مِّنكُم مِّن دِيَٰرِهِمۡ تَظَٰهَرُونَ عَلَيۡهِم بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَإِن يَأۡتُوكُمۡ أُسَٰرَىٰ تُفَٰدُوهُمۡ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيۡكُمۡ إِخۡرَاجُهُمۡۚ أَفَتُؤۡمِنُونَ بِبَعۡضِ ٱلۡكِتَٰبِ وَتَكۡفُرُونَ بِبَعۡضٖۚ فَمَا جَزَآءُ مَن يَفۡعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ إِلَّا خِزۡيٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰٓ أَشَدِّ ٱلۡعَذَابِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Kisha nyinyi hao hao mnauana, na mnalitoa kundi kati yenu katika nyumba zao, mkisaidiana dhidi yao, kwa dhambi na uhasama. Na kama wakikujieni ilhali wakiwa mateka mnawakomboa wakati imeharamishwa kwenu kuwafukuza. Je, mnaamini baadhi ya maandiko na mengine mnayakataa? Basi hakuna malipo kwa mwenye kuyafanya hayo kati yenu isipokuwa tu hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watarejeshwa kwenye adhabu kali zaidi, na Allah si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 86

أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشۡتَرَوُاْ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا بِٱلۡأٓخِرَةِۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Hao ndio walionunua uhai wa dunia kwa Akhera, kwahiyo hawatapunguziwa adhabu na wala hawatanusuriwa



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 87

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَقَفَّيۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ بِٱلرُّسُلِۖ وَءَاتَيۡنَا عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدۡنَٰهُ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِۗ أَفَكُلَّمَا جَآءَكُمۡ رَسُولُۢ بِمَا لَا تَهۡوَىٰٓ أَنفُسُكُمُ ٱسۡتَكۡبَرۡتُمۡ فَفَرِيقٗا كَذَّبۡتُمۡ وَفَرِيقٗا تَقۡتُلُونَ

Na kwa hakika tulimpa Musa Kitabu, na tukafuatishia baada yake kwa kupeleka Mitume, na tukampa Isa Mwana wa Mariamu miujiza iliyo wazi na tukampa nguvu kwa Roho Mtakatifu (Jibrili). Basi je, kila Mtume akikuleteeni yale yasiyopendwa na nafsi zenu mnafanya kiburi? (Mitume) Wengine mliwapinga na wengine mliwaua



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 88

وَقَالُواْ قُلُوبُنَا غُلۡفُۢۚ بَل لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفۡرِهِمۡ فَقَلِيلٗا مَّا يُؤۡمِنُونَ

Na wakasema: Nyoyo zetu zimezibwa. Bali Allah amewalaani kwa kufuru zao, kwa hiyo imani yao ni kidogo mno



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 89

وَلَمَّا جَآءَهُمۡ كِتَٰبٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٞ لِّمَا مَعَهُمۡ وَكَانُواْ مِن قَبۡلُ يَسۡتَفۡتِحُونَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَلَمَّا جَآءَهُم مَّا عَرَفُواْ كَفَرُواْ بِهِۦۚ فَلَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na kilipowafikia Kitabu kito-kacho kwa Allah, kinachothibitisha (yale) waliyokuwa nayo, na huko kabla walikuwa wakiomba nusra dhidi ya wale waliokufuru, basi alipowajia huyo waliye mjua, walimkataa. Basi laana ya Allah iwe juu ya makafiri



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 90

بِئۡسَمَا ٱشۡتَرَوۡاْ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمۡ أَن يَكۡفُرُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بَغۡيًا أَن يُنَزِّلَ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ فَبَآءُو بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٖۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Ni kibaya mno walichojiuzia[1] cha kukataa yale aliyoyateremsha Allah kwa husuda ya kuwa Allah anamteremshia fadhila zake amtakaye miongoni mwa waja wake. Kwa sababu hiyo, walistahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu yenye kudhalilisha


1- - Walichojichagulia


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 91

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ نُؤۡمِنُ بِمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَيَكۡفُرُونَ بِمَا وَرَآءَهُۥ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَهُمۡۗ قُلۡ فَلِمَ تَقۡتُلُونَ أَنۢبِيَآءَ ٱللَّهِ مِن قَبۡلُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na wanapoambiwa: Yaaminini yale aliyoyateremsha Allah, husema: Tunaamini yale tulioteremshiwa na huyapinga yasiyokuwa hayo, nayo ndio haki yenye kuafiki waliyo nayo. Sema: Ni kwanini (mlikuwa) mnawaua Manabii wa Allah hapo zamani kama ninyi ni waumini?



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 92

۞وَلَقَدۡ جَآءَكُم مُّوسَىٰ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ

Na kwa hakika kabisa, alikujieni Musa akiwa na miujiza ya wazi, kisha baada yake[1] mkamfanya Ndama (Mungu) na ilhali nyinyi ni wenye kudhulumu (nafsi zenu)


1- - Baada ya Musa kwenda kwenye kiaga cha kukutana na Mola wake


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 93

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ وَرَفَعۡنَا فَوۡقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱسۡمَعُواْۖ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَعَصَيۡنَا وَأُشۡرِبُواْ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلۡعِجۡلَ بِكُفۡرِهِمۡۚ قُلۡ بِئۡسَمَا يَأۡمُرُكُم بِهِۦٓ إِيمَٰنُكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na (kumbukeni) tulipochukua ahadi yenu na tukauinua (mlima) Turi juu yenu (tukakuambieni): Yashikeni kwa nguvu tuliyokupeni na sikilizeni. Wakasema: Tumesikia na tumeasi, na wakanyweshwa mioyoni mwao (kupenda) kuabudu ndama kwa sababu ya kufuru zao. Waambie: Ni jambo baya sana inavyokuamrisheni imani yenu, kama ninyi ni waumini



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 94

قُلۡ إِن كَانَتۡ لَكُمُ ٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ عِندَ ٱللَّهِ خَالِصَةٗ مِّن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema: Ikiwa makazi ya Akhera (yaliyopo) kwa Allah ni yenu tu kuliko watu wengine, basi tamanini kufa ikiwa nyinyi ni wakweli



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 95

وَلَن يَتَمَنَّوۡهُ أَبَدَۢا بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ

Asilani, hawatalitamani hilo kwa sababu yale yaliyotangulizwa na mikono yao, na Allah anawajua sana wenye kudhulumu



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 96

وَلَتَجِدَنَّهُمۡ أَحۡرَصَ ٱلنَّاسِ عَلَىٰ حَيَوٰةٖ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمۡ لَوۡ يُعَمَّرُ أَلۡفَ سَنَةٖ وَمَا هُوَ بِمُزَحۡزِحِهِۦ مِنَ ٱلۡعَذَابِ أَن يُعَمَّرَۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ

Na kwa hakika kabisa, utawakuta wao (Wayahudi) ndio wanaojali mno uhai[1] kuliko watu wote, na miongoni mwa washirikishaji (pia utakuta nao wako hivyo); anatamani mmoja wao angalau apewe umri wa miaka elfu moja. Na kupewa kwake umri mrefu hakutamuepushia adhabu, na Allah ni Mwenye kuyaona wanayoyatenda


1- - Katika maisha ya duniani


السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 97

قُلۡ مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّـجِبۡرِيلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلۡبِكَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Sema: Mwenye kuwa adui wa Jibrili, basi (ajue kuwa) yeye ndiye aliyeuteremsha Wahyi (Qur’an) moyoni mwako kwa idhini ya Allah, unaosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake na ni muongozo na bishara kwa waumini



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 98

مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّلَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبۡرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوّٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ

Mwenye kuwa adui wa Allah na Malaika wake na Mitume wake na Jibrilina Mikaili, basi hakika, Allah ni adui wa makafiri wote



السورة: AL-BAQARAH 

الآية : 99

وَلَقَدۡ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۖ وَمَا يَكۡفُرُ بِهَآ إِلَّا ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na kwa yakini kabisa, tume-kuteremshia hoja za wazi na hawazikanushi isipokuwa waovu tu